jinsi ya ku download application

0 comments
Ili ufurahie zaidi matumizi ya simu yako ya Android ni vyema kuongeza idadi ya applications au games. Apps nyingi hupatikana bure, lakini nyingine huwa zinauzwa. Kufahamu namna ya kudownload apps zinazouzwa bure soma Jinsi ya kudownload apps zinazouzwa bure Kuna njia nyingi za kudownload apps hizo katika simu yako ya Android.

Njia 3 za kudownload application

1.Google Playstore

Ingia katika app yako ya Google playstore kisha tafuta(search) app uipendayo kisha bonyeza kitufe cha ku-download.
Faida ya ku download apps kwa njia hii ni uhakika wa usalama wako na kifaa chako(simu yako).

2.App store nyingine

Unaweza pia kudownload apps/games kupitia store nyingine kama Amazon store na Mobogenie Store.
Kabla ya ku-install apps kutoka store nyngine kumbuka kuruhusu (apps from unknown sources) nenda
settings>>security>>unknown sources 
kisha washa.

3.Apk katika internet

Njia nyingine ni ya kwenda katika kivinjari(browser) yako na ku-search jina la app yako na mwisho malizia na neno apk mfano facebook apk kisha chagua link moja na ifate kwa ajili ya kudownload.

Kumbuka

Kwa kutumia njia namba 2 na namba 3 hapo juu unaweza kudownload apps fake au zisizo salama kwa simu yako. Inapendekezwa/ni vyema kutumia njia namba 1.