Jinsi ya kudownload video YouTube

0 comments
Jinsi ya kudownload video Youtube limekuwa ni tatizo linalowasumbua watu wengi, licha ya kuwepo njia nyingi sana zinazokuwezesha kudownload video hizo. Nitaongelea njia hizo katika makundi mawili, watumiaji wa simu na kompyuta

Kwa watumiaji wa simu

1.Applications

Unaweza kudownload video za youtube kwa kutumia app katika simu yako. Apps zitakazokuwezesha kudownload zipo , lakini apps hizo hazipatikani Google Playstore kutokana na kwenda kinyume na sheria za Google, mfano
Videorder
Tubemate
Vidmate
Snaptube

2.Youtube app

Kwa kutumia app ya youtube unaweza kudownload kwa sababu wanakupa uwezo wa kufanya hivyo. Tatizo la njia hii video utaweza kuiona kwa kutumia app ya youtube tu.

Kwa watumiaji wa Kompyuta

1.Software

Kuna software kadhaa zitakazofanikisha upatikanaji wa video hizo. Software hizi hazina uhusiano na kampuni ya Youtube na matandao huo upo kinyume na njia zote hizo kutokana na kwamba zinawapunguzia kiwango cha faida wao pamoja mna watengenezaji wa vdeo. Software zenyewe ni kama

4K Video Downloader

Unaweza kuipata software hii free kabisa japo kuna chaguo la kulipia. Kuitumia kudownload ni rahisi kwa ku click na kuna feature ya kuweza kudownload video zote mpya za chanel uliyo subscribe.
Pia ina uwezo wa kuchukua audio(mp3) peke yake bila kudownload video nzima.

WinX YouTube Downloader

Hii inakuwezesha kudownload video za youtube na tovuti nyingine zaidi ya 300. Software hii nayo ni bure kabisa. Kudownload video hapa unaenda katika video unayoihitaji katika tovuti yoyote halafu uta paste kwenye software hiyo na kuanza kudownload video yako pendwa.

5K Player

Hii nayo ni bure moja kwa moja. Unaweza kudownload kutoka katika tovutui zaidi ya 300 na inafanya mambo mengine mengi tofauti a kudownload video. Japo ni ngumu kidogo lakini njia ya kudownload apa ni kama WinX Youtube Downloader unacopy address ya video unayotaka kuichukua kisha unaipaste katika sofftware hii kwa ajili ya kudownload.

Njia kwa ajili ya vyote(simu na kompyuta)

Online download

Unaingia katika website ya kudownload unaweka link ya video unayotaka kuidownload then una download
mfano website
video downloader online
Apowersoft online video downloader
Clip convertor

Internet direct

hapa ukitumia browser yako kawaida baada ya kufika katika video unayotaka kudownload unaongeza ss katika link ya video yako kisha unafuata maelekezo kudownload
mfano kwenye link https://www.youtube.com/dsjbkj…… inakua https://www.ssyoutube.com/dsjbk

Naanini umepata uelewa katika namna moja au nyingine kuhusu jinsi ya kudownload video Youtube. Kama una swali au maoni yoyote usisite kuacha comment yako hapo chini.