Jinsi ya kupunguza tumbo

0 comments
Kitu chochote kikizidi kupita kiasi cha kawaida huwa ni hatari, vivyo hivyo kuwa na kitambi inaweza kuwa hatari kwa afya. Hatari zinaweza kuwa kupata shinikizo la damu, magonjwa ya moyo na saratani kama saratani ya matiti au tumbo.

Sababu za tatizo hili zinaweza kuwa kula kupita kiasi, uzee au matumizi ya pombe.

Jinsi ya kupunguza tumbo

1.Fanya  mazoezi.

Tenga mda wa kufanya mazoezi angalau siku tano katika wiki. Unaweza kutumia dakika zisizopungua 30 kila siku kuhakikisha unatokwa na jasho la kutosha.

Mazoezi yanaweza kuwa
  • kutembea
  • kukimbia
  • programu maalum za 'gym'

2.Pangilia chakula

Pangilia unachokula kila siku.Kula milo yote yaani asubuhi, mchana na jioni kwa sababu kushindwa kufanya hivyo kunaweza kupelekea kula kupita kiasi mlo unaofata.

Zingatia
  • kula mboga nyingi za majani, zitakufanya ujisikie umeshiba na hivyo utakula kidogo
  • kula zaidi vyakula vyenye protini kama nyama, samaki, mayai na maharage
  • epuka vyakula vyenye sukari nyingi
  • epuka vinywaji vyenye sukari nyingi mfano soda
  • epuka kunywa pombe kupita kiasi

3.Pata usingizi wa kutosha

Hakikisha unapata usingizi wa kutosha kila siku angalau  masaa 7 au 8. Kupata usingizi wa kutosha kunaweza kusaidia kupunguza msongo wa mawazo.

4.Punguza msongo wa mawazo(stress)

Jiepushe na mambo yanayoweza kupelekea msongo wa mawazo. Pata usingizi wa kutosha, jichanganye katika makundi ya watu kama marafiki, fanya mazoezi na epuka matumizi ya pombe na 'caffeine' ku-deal na tatizo la msongo wa mawazo.

5.Zaidi

Jaribu kufunga. kunaweza kukusaidia kupambana na matumizi yako ya chakula

Dondoo

>Hakuna njia au dawa ya maajabu ya kupunguza tumbo. Matumizi ya njia hizo au mchanganyiko wa njia hizo zinaweza kufanya kazi kabisa
>Jiwekee malengo ya kutimiza na uhakikishe umetimiza mfano kujenga mwili wa mazoezi.