Jinsi ya kuomba

2 comments
Tunapaswa kuomba kila wakati, wakati tukiwa na shida au raha, mchana au usiku, milimani na mabondeni. Tunatakiwa kufahamu kuwa kuomba ni kuzungumza na Mungu. Na tukiomba tutapokea. "Niite, nami nitakuitikia" Yeremia 33:3  "Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza." Yeremia 29:12

Jinsi ya kuomba

1.Sifu

Msifu Mungu kwa mambo makuu anayoyatenda kila siku. Msifu katika nyimbo au kwa kutaja maneno yenye kuonesha ukuu wake kati ya watu wote. "Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana. Haleluya." Zaburi 150:6 "Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake." Waebrania 13:15

2.Tubu

Tubu dhambi zako ulizozifanya (zile unazofahamu na usizofahamu) kwa sababu atakusamehe. "Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote." 1Yohana 1:9.

3.Shukuru

Mshukuru Mungu kwa sababu ya baraka zake anazokupatia. Mshukuru kwa sababu ya vitu vikubwa na vidogo, vizuri na vibaya, na kila kitu kinachotokea maishani mwako. "Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele." 1Mambo ya Nyakati 16:34.

4.Mahitaji

Fikisha mahitaji yako kwa Mungu kwani ni baba yako na atakusikiliza na kukupa majibu kutokana na mahitaji yako. "Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu." Wafilipi 4:6.

Zaidi

  • amini kuwa Mungu anakusikia na atakujibu
  • soma Biblia
  • tambua lengo lako la kuomba
  • tafuta eneo zuri kwa ajili ya kuomba
  • "Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;" Mathayo 7:7.
  • Fanya maombi kuwa sehemu ya maisha yako
  • Ombea wengine.
 

Dondoo

>Sio lazima kuwa sehemu tulivu au kanisani kwa ajili ya kuomba, unaweza kuomba ukiwa popote