Jinsi ya kujiajiri

0 comments

Ili kujiajiri unapaswa kuzingatia mambo yafuatayo


1.Jifahamu

Jitathmini kipi ulichonacho. Hapa inamaanisha tambua ujuzi ulio nao na kama ujuzi huo unaweza kusababisha kutengeneza huduma au bidhaa. Ujuzi unaweza kuwa elimu uliyoipata chuo au shule au uzoefu wowote uliopata katika maisha ya kila siku mfano kutengeneza kompyuta, kupika, au kufundisha.

Pia unahitahji kuangalia hamasa uliyonayo katika sehemu uliyo na ujuzi mfano kama una ujuzi wa kufundisha na una hamasa kubwa ya kazi hiyo kiasi kiwamba unaweza ukaifanya bila hata kulipwa. Pia unaweza kuwa na hamasa iliyopitiliza katika kitu fulani umbacho huna ujuzi nacho, hapa unaweza kutafuta njia ya kujifunza ujuzi huo.

Matatizo mbalimbali yanayowasumbua watu yanaweza kukufanya upate wazo utakalolitumia mfano tatizo la joto ndio sababu ya uwepo wa biashara ya feni.

Mpaka hapo unaweza kuja na wazo la biashara utakayotaka kufanya.

2.Chambua vizuri wazo lako

Ukiwa tayari umepata wazo la biashara unayohitaji kufanya(kwa kutumia hatua ya kwanza hapo juu) fuata hatua chache kuchambua wazo lako.

Angalia
  • Ni watu gani watakuwa wateja wako?
  • Washindani wako ni wa kina nani?

3.Andaa mpangokazi wa biashara yako

Hapa utagundua vitu kama
  • kiasi gani cha mtaji kitahitajika
  • Utahitaji mda gani kwa biashara kuanza kuleta faida
  • Ni vikwazo gani unaweza kukutana navyo
  • Ni eneo gani litatumika kwa ajili ya biashara

4.Tafuta mtaji

Kutokana na wazo na mpango kazi wa biashara yako utakua umekwisha kujua utahitaji mtaji kiasi gani. Unaweza kupata mtaji kwa njia mbalimbali kama
  • Akiba yako uliyonayo
  • Mkopo kutoka kwa ndugu au rafiki
  • Mkopo kutoka taasisi za kifedha kama benki

5.Sajili biashara yako

Fata taratibu zilizowekwa na nchi kwa kusajili biashara yako. Sajili jina la biashara yako kisha biashara yenyewe kama taratibu zinavyokuhitaji wewe kufanya

6.Anza biashara

Apa ndiyo sehemu yenye kufurahisha zaidi. Tumia eneo ulilopanga anza kufanya kazi kama ulivyopanga katika mpangokazi wako. Unaweza pia kufanya sherehe ya ufunguzi rasmi ili kutoa taarifa kuwa umeanza kutoa huduma

7.Ziada

Inaweza kukuchukua muda kugundua njia sahihi za wewe kufanya biashara yako kwa ufanisi mkubwa, unachotakiwa kufanya ni kufata mpango kazi wako lakini badilika kulingana na mazingira. Pia
  • Fanya matangazo
  • chunguza soko lako
  • tumia teknolojia ya kisasa kwa faida yako
 

Dondoo

>"Kitu unachopenda sana na ungependa ufanye kila siku" maneno hayo yanaweza kukusaidia kufahamu aina ya biashara unayoweza kufanya

>Kutafuta njia ya kutatua matatizo ya kila siku inaweza kuwa njia ya kupata wazo la biashara

>Kujua jinsi ya kujiajiri na kuchukua hatua kutakusaidia wewe na wengine wengi(wa Tanzania na wengine) baada ya wewe kufanikiwa.