Kuna njia kadhaa za kudownload na ku install whatsapp kwenye simu yako ya android.
Njia 3 za kudownload na ku install whatsapp
- Google Playstore
Ingia katika app yako ya Google playstore kisha tafuta kwa kuandika neno whatsapp kisha bonyeza kitufe cha ku-download.
Faida ya kudownload kwa njia hii ni uhakika wa usalama wako na kifaa chako(simu yako). - Whatsapp website
Ingia katika browser yako kisha nenda whatsapp.com halafu fuata maelekezo kwa ajili ya kudownload.
- App store nyingine
Unaweza pia kudownload kupitia app store nyingine kama Amazon store na Mobogenie Store.
Kumbuka
Kabla ya ku-install kwa kutumia njia namba 2 na 3 kumbuka kuruhusu (apps from unknown sources) nenda
settings>>security>>unknown sources
kisha washa.