Jinsi ya kuunganisha internet kwenye computer

0 comments
Njia zote kwa ufupi 
  1. Mobile Hotspot 
  2. USB Tethering.
  3. Bluetooth Tethering.
  4. Modem
  5. WIFI
(Kwa namba 1,2 na 3 lazima uwe na simu yenye uwezo wa internet).

1. MOBILE HOTSPOT.

  • Fungua simu yako SETTINGS>>MORE NETWORKS>>TETHERING AND PORTABLE HOTSPOT>>PORTABLE WI-FI HOTSPOT(BONYEZA ON).
  • Fungua computer yako OPEN NETWORK AND SHARING CENTER. Hapo utaona jina la hotspot yako kisha utaibonyeza na kujiunga nayo, kama kuna password utaziingiza na kisha bonyeza enter. Sasa unaweza kufunungua internet na kuperuzi.

2. USB TETHERING.

HAKIKISHA UNA WAYA WA USB KWA AJILI YA KUUNGANISHA SIMU NA COMPUTER YAKO. Chomeka simu yako kwenye computer yako kwa kutumia usb waya na hakikisha simu yako inasoma kwenye computer yako.

  • Fungua simu yako SETTINGS>>MORE NETWORKS>>TETHERING AND PORTABLE HOTSPOT>>USB TETHERING(BONYEZA ON). Baada ya sekunde chache utaweza kutumia internet ya simu yako kwenye computer yako. 
 

3. BLUETOOTH TETHERING.

  • Fungua simu yako SETTINGS>>MORE NETWORKS>>TETHERING AND PORTABLE HOTSPOT>>BLUETOOTH TETHERING(WEKA ON)
  • Fungua computer yako CONTROL PANEL>>HARDWARE AND SOUND>>DEVICES AND PRINTERS. Hapa utaiona simu yako kwenye computer yako kisha right click kwenye hiyo simu yako itatokea "connect using" bonyeza "access point". Bluetooth itaunganisha internet kwenye computer yako.

MUHIMU:Katika njia zote tatu hapo juu USB Tethering ndio njia ya haraka zaidi kuliko Bluetooth Tethering na Mobile Hotspot.

4.MODEM

  • Hapa lazima uwe na kifaa kinachoitwa modem(bei yake inaanzia 20,000). Unaweka laini katika hiyo modem alafu unachomeka katika kompyuta yako ili uweze kutumia internet
  • Utapata maelekezo jinsi ya kuitumia pale utakaponunua.

5. WIFI

  • Hii ni kama njia ya hotspot pale juu sema naiongelea kwa kuhusisha WIFI zinazotolewa na kampuni, mashirika au sehemu zozote au kutoka kwa wanaomiliki vifaa kama routers.
  • Unachotakiwa kufanya hapa ni kuwasha WIFI kuangalia kama kutakuwa na inayopatikana kwa muda huo kisha una connect. Mara nyingi zinakua na password hivyo ni vyema kufahamu password kwanza.