Kutunza taarifa za vitu mbalimbali ni muhimu. Chaguo la kupiga picha screen yako linaweza kuwa la kwanza kwa wakati ukiwa unatumia applications nyingine kama facebook nk. Kujua jinsi ya ku screenshot kunaweza kuokoa muda wako.
Unaweza kutumia njia zifuatazo ili kupiga screenshot
- Kutumia power button pamoja na button ya kupunguzia sauti
Shikilia kwa pamoja button ya kuwasha/kuzima simu pamoja na ya kupunguzia sauti kwa muda kidogo mpaka utakapoona picha yako ikitokea.
- Kutumia chaguo lililopo katika notification bar.
Unaweza pia kutumia chaguo lililopo katika simu yako ya android kwa kuangalia moja kwa moja katika notification bar na kisha kubonyeza screenshot. Angalia picha chini.
- Kutumia apps zinazopatikana playstore.
Pia unaweza kupata apps mbalimbali katika google playstore zinazoweza kukuwezesha kupiga picha screen yako kwa urahisi. Kujua jinsi ya kudownload app soma hii Jinsi ya kudownload apps/games kwenye simu ya android.