Jinsi ya kutengeneza page ya Facebook

3 comments
Huenda umekuwa ukijiuliza kama kuna faida yoyote ya kuwa na kurasa(page) ya facebook. Napenda kukujuza kuwa kuna faida kubwa ya kuwa na ukurasa wa facebook. Moja ya faida ikiwa ni eneo la kukutana na wateja wa bidhaa au huduma yako.

Hatua za kufata kufungua page yako

KOMPYUTA

  • Ingia katika kivinjari(browser) yako kisha ingia katika tovuti ya facebook kisha fungua acccount(sign up) au ingia katika account yako(log in)
  • Bonyeza sehemu iliyoandikwa 'Create' kisha bonyeza neno 'Page' lililo chini yake
 


  • Hatua inayofata ni kuchagua aina ya page unayotaka kufungua. Kwa mfano mimi nimechagua "business or brand". Chagua 'Business or Brand' kama unataka kufungua page kwa ajili ya biashara na 'Community au Public Figure' kama unataka kufungua page kwa ajili ya kikundi au mtu maarufu.




  • Baada ya hapo andika jina la page unayotaka kufungua kwenye sehemu inayouliza 'Page Name' na jaza category ya page unayotaka kufungua kisha bonyeza 'Continue'
  • Mpaka hapo unakua umemaliza kufungua page yako. Unaweza kuendelea na hatua zinazofata au ukaachana nazo kwa kubonyeza neno 'SKIP' 

SIMU(KWA KUTUMIA FACEBOOK APP)

  • Ingia katika app yako ya facebook. Kama bado hauja download Facebook, angalia hapa njia za kudownload. (hakikisha umejiunga au umeigia katika akaunti yako ya facebook) kisha bonyeza alama ya mistari mitatu iliyopo juu pembeni ya sehemu ya 'notifications' kisha tafuta neno create a page na ubonyeze neno hilo



  • Baaada ya kubonyeza neno hilo itatookea page kama inaayoonekana hapo chini. Bonyeza 'Get Started'

  • Andika jina kwa ajili ya page yako mfano 'Mojasky tz'

  • Kisha chagua aina na aina ndogo ya page zako (angalia mfano katika picha chini) kisha bonyeza neno 'NEXT' kumaliza hatua za kufungua page yako. 

  • Unaweza kuendelea na machaguo yanayofata au unaweza kuacha na ukafanya badae kwa kubonyeza neno 'SKIP' (Machaguo yanayofata ni kama ku-upload profile picha au picha ya kava)

Kuwa na ukurasa wa facebook peke yake haitoshi, ni vyema pia ukawa na website/blog kwa sababu hauwezi kujua ni lini facebook watafanya mabadiliko yatakayosababisha wewe kupata tatizo la mawasiliano na wateja wako. Kumiliki tovuti au blog hakutakuhitaji wewe kufahamu jinsi ya kutengeneza. Unaweza kupata ushauri kutoka HAPA